Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 60. Je! wale ambao hawajawahi kusikia injili na kwa hiyo hawamjui Yesu Kristo wala kumwamini wanaweza kuokolewa kwa namna yao ya kuishi kulingana na nuru ya asili?
J. Wale ambao hawajawahi kusikia injili, wasiomjua Yesu Kristo, wala kumwamini, hawawezi kuokolewa, ingawa wanajitahidi kurekebisha maisha yao kwa nuru ya asili, na kwa sheria za dini wanazozikiri, wala hakuna wokovu kwa mtu mwingine yeyote ila tu katika Kristo, ambaye ndiye mwokozi pekee wa mwili wake, yaani Kanisa.
- Warumi 10:14.
- 2 Wathesalonike 1:8,9.
- Waefeso 2:12.
- Yohana 1:10-12.
- Yohana 8:24.
- Marko 16:16.
- 1 Wakorintho 1:20-24.
- Yohana 4:22.
- Warumi 9:31,32.
- Wafilipi 3:4-9.
- Matendo 4:12.
- Waefeso 5:23.