Inapakia

Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo

Sw. 37. Kristo, akiwa Mwana wa Mungu, alikuwaje mwanadamu?

J. Kristo, Mwana wa Mungu, alikuwa mwanadamu kwa kujitwalia mwili wa kweli na nafsi yenye akili, akiwa ametungwa mimba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu tumboni mwa Bikira Maria, kutoka katika dhati yake, na kuzaliwa naye, lakini pasipo dhambi.
  • Yohana 1:14.
  • Mathayo 26:38.
  • Luka 1:27,31,35,42.
  • Wagalatia 4:4.
  • Waebrania 4:15.
  • Waebrania 7:26.