Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 89. Ni nini kitatendeka kwa waovu siku ya hukumu?
J. Siku ya hukumu waovu watawekwa upande wa kushoto wa Kristo na kwa ushahidi wazi na kwa usadikisho kamili wa dhamiri zao wenyewe, watapokea hukumu ya kutisha lakini ya haki ya adhabu iliyotamkwa dhidi yao, na kisha watatupwa nje ya uwepo wenye neema wa Mungu, na ushirika wenye utukufu wa Kristo, wa watakatifu wake, na wa malaika wote watakatifu, na waende kuzimu ambapo wataadhibiwa kwa mateso yasiyoelezeka katika mwili na nafsi, pamoja na shetani na malaika wake milele.
- Mathayo 25:33.
- Warumi 2:15,16.
- Mathayo 25:41-43.
- Luka 16:26.
- 2 Wathesalonike 1:8,9.