Muhtasari wa Majukumu ya Kikristo
Sw. 96. Ni nini manufaa hasa ya sheria kwa watu ambao hawajazaliwa upya?
J. Sheria ya maadili ni ya manufaa kwa watu ambao hawajazaliwa upya kwa kuamsha dhamiri yao ili wakimbie hasira itakayokuja, kuwaelekeza kwa Kristo, au wakiendelea katika hali na njia ya uovu, kuwafanya wasiwe na udhuru, na chini ya laana yake.
- 1 Timotheo 1:9,10.
- Wagalatia 3:24.
- Warumi 1:20.
- Warumi 2:15.
- Wagalatia 3:10.