Inapakia

Njia za Neema na Ibada

Sw. 161. Sakramenti zinakuaje njia zenye ufanisi za wokovu?

J. Sakramenti zinakuwa njia zenye ufanisi za wokovu, si kwa nguvu yoyote iliyomo ndani yake wala kwa wema wowote unaotokana na uchaji Mungu au nia ya yeye anayezisimamia, bali tu kwa utendaji wa Roho Mtakatifu na baraka za Kristo aliyezianzisha.
  • 1 Petro 3:21.
  • Matendo 8:13,23.
  • 1 Wakorintho 3:6,7.
  • 1 Wakorintho 12:13.