Inapakia

Njia za Neema na Ibada

Sw. 189. Utangulizi wa Sala ya Bwana unatufundisha nini?

J. Utangulizi wa Sala ya Bwana (ulio katika maneno haya: Baba yetu uliye mbinguni), unatufundisha kwamba tunapoomba tumkaribie Mungu kwa kutumainia wema wake wa baba na ushiriki wetu ndani yake, kwa staha na tabia nyingine zote za kiwanafsi, hisia za mbinguni na mtambuo sahihi wa uweza wake mkuu, ukuu wake na kujishusha kwake kwa rehema, pamoja na kuomba pamoja na wengine na kwa ajili ya wengine.
  • Mathayo 6:9.
  • Luka 11:13.
  • Warumi 8:15.
  • Isaya 64:9.
  • Zaburi 123:1.
  • Maombolezo 3:41.
  • Isaya 63:15,16.
  • Nehemia 1:4-6.
  • Matendo 12:5.