Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 35. Agano la neema linatekelezwaje chini ya Agano Jipya?
J. Chini ya Agano Jipya, Kristo mwenye dhati yenyewe alipokwisha kudhihirishwa, agano lilelile la neema lilitekelezwa na bado linatekelezwa kwa kuhubiriwa kwa Neno, na kwa kutumika kwa sakramenti za ubatizo na Meza ya Bwana; ambamo neema na wokovu vinaonyeshwa kwa ukamilifu zaidi, uwazi zaidi, na nguvu zaidi, kwa mataifa yote.
- Marko 16:15.
- Mathayo 28:19,20.
- 1 Wakorintho 11:23-25.
- 2 Wakorintho 3:6-9.
- Waebrania 8:6,10,11.
- Mathayo 28:19.