Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 34. Agano la neema lilitekelezwaje chini ya Agano la Kale?
J. Agano la neema lilitekelezwa chini ya Agano la Kale kwa njia ya ahadi, unabii, dhabihu, tohara, pasaka, na alama na maagizo mengine, ambayo yote yalimwashiria kimbele Kristo atakayekuja, na yalitosha kwa wakati huo kuwajenga wateule katika imani kwa Masihi aliyeahidiwa, ambaye kwake walikuwa na msamaha kamili wa dhambi na wokovu wa milele.
- Warumi 15:8.
- Matendo 3:20,24.
- Waebrania 10:1.
- Warumi 4:11.
- 1 Wakorintho 5:7.
- Waebrania 8-10.
- Waebrania 11:13.
- Wagalatia 3:7-9,14.