Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 30. Je! Mungu aliwaacha wanadamu wote kuangamia katika hali yao ya dhambi na taabu?
J. Mungu hakuwaacha wanadamu wote kuangamia katika hali yao ya dhambi na taabu, ambamo walianguka kwa kuvunja agano la kwanza, linaloitwa kwa kawaida agano la matendo, bali kwa upendo wake safi na rehema yake aliwakomboa wateule wake, akawatoa katika hali hiyo na kuwaingiza katika hali ya wokovu kwa njia ya agano la pili linaloitwa agano la neema.
- 1 Wathesalonike 5:9.
- Wagalatia 3:10,12.
- Tito 3:4-7.
- Wagalatia 3:21.
- Warumi 3:20-22.