Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 80. Je! waamini wa kweli wanaweza kuwa na uhakika usio na shaka kwamba wako katika hali ya neema na kwamba wataendelea humo mpaka wokovu?
J. Wote walio waamini wa kweli katika Kristo na wanajitahidi kutembea kwa dhamiri njema yote mbele zake, wanaweza, bila ufunuo wa pekee, kwa imani inayotegemea ukweli wa ahadi za Mungu na kwa uwezo anaowapa Roho kutambua ndani yao neema hizo ambazo ahadi za uzima zimefanywa, na kuwapa ushuhuda pamoja na roho zao kwamba wao ni watoto wa Mungu, wanaweza kuwa na uhakika usiokosea kwamba wako katika hali ya neema na kwamba wataendelea humo mpaka wokovu.
- 1 Yohana 2:3.
- 1 Wakorintho 2:12.
- 1 Yohana 3:14,18,19,21,24.
- 1 Yohana 4:13,16.
- Waebrania 6:11,12.
- Warumi 8:16.
- 1 Yohana 5:13.