Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 79. Je! waamini wa kweli hawawezi, kwa sababu ya kutokamilika kwao, na majaribu mengi na dhambi wanazokumbana nazo, kuanguka kutoka hali ya neema?
J. Waamini wa kweli, kwa sababu ya upendo usiobadilika wa Mungu, amri yake na agano lake la kuwapa uvumilivu, muungano wao usiotengana na Kristo, maombezi yake ya daima kwa ajili yao, na Roho na mbegu ya Mungu inayokaa ndani yao, hawawezi kuanguka wala kamwe kabisa kutoka hali ya neema, bali watalindwa kwa uweza wa Mungu kwa njia ya imani kwa wokovu.
- Yeremia 31:3.
- 2 Timotheo 2:19-21.
- 2 Samweli 23:5.
- 1 Wakorintho 1:8,9.
- Waebrania 7:25.
- Luka 22:32.
- 1 Yohana 2:27.
- 1 Yohana 3:9.
- Yeremia 32:40.
- Yohana 10:28.
- 1 Petro 1:5.