Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 22. Je! wanadamu wote walianguka katika kosa lile la kwanza?
J. Kwa kuwa agano lilifanywa na Adamu kama mtu wa umma, si kwa ajili yake tu bali pia kwa ajili ya wazao wake, wanadamu wote, wanaotokana naye kwa njia ya kawaida ya uzazi, l) walitenda dhambi ndani yake na wakaanguka pamoja naye katika kosa la kwanza. ll)
- Matendo 17:26.
- Mwanzo 2:16-17.
- Warumi 5:12-20.
- 1 Wakorintho 15:21-22.