Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 32. Neema ya Mungu inajidhihirishaje katika agano la pili?
J. Neema ya Mungu inajidhihirisha katika agano la pili, kwa kuwa Mungu kwa uhuru amewapatia wenye dhambi mpatanishi, l) pamoja na uzima na wokovu kwa njia yake, ll) akidai imani kama sharti la wao kushiriki ndani yake, m) akiahidi na kutoa Roho wake Mtakatifu kwa wateule wake wote, n) akifanya ndani yao imani, ñ) na neema nyingine zote ziokoazo, o) akiwawezesha kwa ajili ya utii wote mtakatifu, p) kama ushahidi wa ukweli wa imani yao na shukrani zao kwa Mungu, na kama njia aliyowawekea kwa wokovu.
- Mwanzo 3:15.
- Isaya 42:6.
- Yohana 6:27.
- 1 Yohana 5:11-12.
- Yohana 1:12.
- Yohana 3:16.
- Mithali 1:23.
- 2 Wakorintho 4:13.
- Wagalatia 5:22-23.
- Ezekieli 36:27.
- Yakobo 2:18,22.
- 2 Wakorintho 5:14-15.
- Waefeso 2:18.