Muhtasari wa Mafundisho ya Kikristo
Sw. 16. Je! dhambi ya babu zetu wa kwanza iliangukia wanadamu wote?
J. Agano lilipofanywa na Adamu, si kwa ajili yake tu, bali pia kwa ajili ya wazao wake; wanadamu wote, wanaotokana naye kwa njia ya kawaida ya uzazi, walitenda dhambi ndani yake, na wakaanguka pamoja naye katika kosa lake la kwanza.
- Mwanzo 2:16-17.
- Yakobo 2:10.
- Warumi 5:12-21.
- 1 Wakorintho 15:22.