Inapakia

Swali Tunaomba nini katika ombi la tano? la Katekisimo Ndogo ya Westminster

Swali Tunaomba nini katika ombi la tano? la Katekisimo Ndogo ya Westminster - jibu pamoja na marejeo ya Biblia
Sw. 105. Tunaomba nini katika ombi la tano?
J. Katika ombi la tano linalosema: "Tusamehe deni zetu, kama sisi nasi tunavyowasamehe wadeni wetu", tunaomba kwamba Mungu, kwa upendo wa Kristo, atusamehe bure dhambi zetu zote; na tunahimizwa kuomba hili, kwa sababu kwa neema yake, tunajiona tayari kusamehe wengine kwa dhati.
  • Zaburi 51:1-2,7,9.
  • Danieli 9:17-19.
  • 1 Yohana 1:7.
  • Mathayo 18:21-35.
  • Waefeso 4:32.
  • Wakolosai 3:13.