Sw. 35. Kutakaswa ni nini?
J. Kutakaswa ni kazi ya neema ya bure ya Mungu, ambayo kwa hiyo tunafanywa upya katika mtu wetu wote kwa mfano wa Mungu, na kuwezeshwa zaidi na zaidi kufa kwa dhambi na kuishi katika haki.
- Ezekieli 36:27.
- Wafilipi 2:13.
- 2 Wathesalonike 2:13.
- 2 Wakorintho 5:17.
- Waefeso 4:23-24.
- 1 Wathesalonike 5:23.
- Ezekieli 36:25-27.
- Warumi 6:4,6,12-14.
- 2 Wakorintho 7:1.
- 1 Petro 2:24.